BETI NASI UTAJIRIKE

CHELSEA: COSTA ULICHOKOZA MOTO KUWA MVUMILIVU

Diego Costa huna nafasi tena chelsea maana unakoelekea inawezekana ikawa mwisho wako kisoka uingereza

Diego Costa anaendelea kukalia kuti kavu darajani na hii imedhibitika leo baada ya uongozi wa chelsea kuamuru gari lake lisipaki yanapopaki magari mengine ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na sasa ameambiwa atapaki wanapofanyia mazoezi watoto wa timu B

   Diego costa mchezaji aliyeongoza kwa magoli mengi ya kufunga msimu wa2013/14 kwa klabu ya Atletico madrid huku akifunga magoli 27 kati ya michezo 35 na kuipa ubingwa wa La Liga timu yake ya Atletico madrid pia aliisaidia timu hiyo kuingia UEFA fainali ingawa walifungwa na yeye alicheza dakika 9 tu. Jose mourinho akiwa chelsea  alimnunua kwa kiasi cha euro milioni 32 msimu wa 2014/15 alicheza michezo 26 na kufunga magoli 20 msimu wa 2015/16 alicheza michezo 28 akifunga magoli 12 na msimu wa  2016/17 amecheza michezo 35 na kufunga magoli 20 msimu huu wa 2017/18 hajacheza mchezo woote .akiwa na   chelsea amefunga  jumla ya magoli 52

                  diego costa akiwa katika gari lake la kifahari Range Rover vogue 2015 autobiograph

ikumbukwe msimu wa 2015/16 na 2016/17 costa amekuwa mfungaji bora wa klabu na ameisaidia chelsea kubeba EPL msimu wa2016/17.
sekeseke lake lilianza kwa  kocha antonio conte kutomjumuisha na  hana mipango nae msimu huu wa 2017/18 na atafute timu nyingine. Costa alisisitiza kutaka kurudi  kujiunga na miamba ya soka na klabu  yake ya zamani  Atletico madrid ,aidha costa alikataa ofa za timu nyingine na kutaka kurudi Atletico Madrid ambayo ilifungiwa kutosajili wachezaji kwa kipindi cha miaka miwili na adhabu hiyo itakwisha 2018.
kitendo cha kuondolewa kwa gari lake na kupelekwa timu B kinadhihirisha costa hatacheza mechi yoyote ya ligi msimu huu hivyo awe mvumilivu kwa yanayoendelea

Post a Comment

0 Comments